Mithali 20:3
Proverbs 20:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ni kwa heshima ya mtu kujitenga ugomvi, bali kila mpumbavu ni mwepesi kugombana.
Proverbs 20:3 in English
Proverbs 20:3 · Berean Standard Bible
It is honorable for a man to resolve a dispute, but any fool will quarrel.
Context
1Mvinyo ni mdhihaki na kileo ni mgomvi;
yeyote apotoshwaye navyo hana hekima. 2Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba;
yeye amkasirishaye hupoteza uhai wake. 3Ni kwa heshima ya mtu kujitenga ugomvi,
bali kila mpumbavu ni mwepesi kugombana. 4Mvivu halimi kwa majira;
kwa hiyo wakati wa mavuno hutazama
lakini hapati chochote. 5Makusudi ya moyo wa mwanadamu ni maji yenye kina,
lakini mtu mwenye ufahamu huyachota.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.