Mithali 18:21
Proverbs 18:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi, nao waupendao watakula matunda yake.
Proverbs 18:21 in English
Proverbs 18:21 · Berean Standard Bible
Life and death are in the power of the tongue, and those who love it will eat its fruit.
Context
19Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuridhika
kuliko mji uliozungushiwa ngome,
nayo mabishano ni kama malango
ya ngome yenye makomeo. 20Tumbo la mtu litajaa kutokana na tunda la kinywa chake,
atashibishwa mavuno yanayotokana na midomo yake. 21Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi,
nao waupendao watakula matunda yake. 22Apataye mke apata kitu chema
naye ajipatia kibali kwa Bwana. 23Mtu maskini huomba kuhurumiwa
bali tajiri hujibu kwa ukali.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.