Mithali 17:10
Proverbs 17:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Karipio humwingia sana mtu mwenye kutambua kuliko mapigo mia kwa mpumbavu.
Proverbs 17:10 in English
Proverbs 17:10 · Berean Standard Bible
A rebuke cuts into a man of discernment deeper than a hundred lashes cut into a fool.
Context
8Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho;
kokote kigeukiapo, hufanikiwa. 9Yeye anayesamehe kosa hudumisha upendo,
bali yeyote arudiaye jambo hutenganisha marafiki wa karibu. 10Karipio humwingia sana mtu mwenye kutambua
kuliko mapigo mia kwa mpumbavu. 11Mtu mbaya hupenda kuasi tu;
mjumbe asiye na huruma atatumwa dhidi yake. 12Ni afadhali ukutane na dubu aliyenyangʼanywa watoto wake,
kuliko mpumbavu katika upumbavu wake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.