Mithali 15:16
Proverbs 15:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Afadhali kuwa na kidogo pamoja na kumcha Bwana, kuliko mali nyingi pamoja na ghasia.
Proverbs 15:16 in English
Proverbs 15:16 · Berean Standard Bible
Better a little with the fear of the LORD than great treasure with turmoil.
Context
14Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa,
bali kinywa cha mpumbavu hujilisha upumbavu. 15Siku zote za wanaoonewa ni za taabu,
bali moyo mchangamfu una karamu ya kudumu. 16Afadhali kuwa na kidogo pamoja na kumcha Bwana,
kuliko mali nyingi pamoja na ghasia. 17Afadhali chakula cha mboga mahali palipo na upendo
kuliko nyama ya ndama iliyonona pamoja na chuki. 18Mtu mwepesi wa hasira huchochea ugomvi,
bali mtu mvumilivu hutuliza ugomvi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.