Native Bible

Proverbs 14:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yeye anayemdharau jirani yake hutenda dhambi, bali amebarikiwa yeye aliye na huruma kwa mhitaji.

Proverbs 14:21 in English

Proverbs 14:21 · Berean Standard Bible

He who despises his neighbor sins, but blessed is he who shows kindness to the poor.

Context

19Watu wabaya watasujudu mbele ya watu wema, nao waovu kwenye malango ya wenye haki. 20Maskini huepukwa hata na majirani zao, bali matajiri wana marafiki wengi. 21Yeye anayemdharau jirani yake hutenda dhambi, bali amebarikiwa yeye aliye na huruma kwa mhitaji. 22Je, wale wanaopanga ubaya hawapotoki? Bali wale wanaopanga kilicho chema hupata upendo na uaminifu. 23Kazi zote zinazofanywa kwa bidii huleta faida, bali mazungumzo matupu huelekea umaskini tu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.