Mithali 14:22
Proverbs 14:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Je, wale wanaopanga ubaya hawapotoki? Bali wale wanaopanga kilicho chema hupata upendo na uaminifu.
Proverbs 14:22 in English
Proverbs 14:22 · Berean Standard Bible
Do not those who contrive evil go astray? But those who plan goodness find * loving devotion and faithfulness.
Context
20Maskini huepukwa hata na majirani zao,
bali matajiri wana marafiki wengi. 21Yeye anayemdharau jirani yake hutenda dhambi,
bali amebarikiwa yeye aliye na huruma kwa mhitaji. 22Je, wale wanaopanga ubaya hawapotoki?
Bali wale wanaopanga kilicho chema
hupata upendo na uaminifu. 23Kazi zote zinazofanywa kwa bidii huleta faida,
bali mazungumzo matupu huelekea umaskini tu. 24Utajiri wa wenye hekima ni taji yao,
bali upumbavu wa wapumbavu huzaa upumbavu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.