Mithali 14:18
Proverbs 14:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mjinga hurithi upumbavu, bali wenye busara huvikwa maarifa kichwani kama taji.
Proverbs 14:18 in English
Proverbs 14:18 · Berean Standard Bible
The simple inherit folly, but the prudent are crowned with knowledge.
Context
16Mtu mwenye hekima humcha Bwana na kuepuka mabaya,
bali mpumbavu hukasirika kwa hamaki na uzembe. 17Mtu anayekasirika kwa haraka hufanya mambo ya upumbavu,
naye mtu wa hila huchukiwa. 18Mjinga hurithi upumbavu,
bali wenye busara huvikwa maarifa kichwani kama taji. 19Watu wabaya watasujudu mbele ya watu wema,
nao waovu kwenye malango ya wenye haki. 20Maskini huepukwa hata na majirani zao,
bali matajiri wana marafiki wengi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.