Mithali 11:26
Proverbs 11:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watu humlaani mtu awanyimae watu nafaka, bali baraka itamkalia kichwani kama taji yeye aliye radhi kuiuza.
Proverbs 11:26 in English
Proverbs 11:26 · Berean Standard Bible
The people will curse the hoarder of grain, but blessing will crown the one who sells it.
Context
24Kuna mtu atoaye kwa ukarimu, hata hivyo hupata zaidi,
mwingine huzuia, lakini huwa maskini. 25Mtu mkarimu atastawi;
yeye awaburudishaye wengine
ataburudishwa mwenyewe. 26Watu humlaani mtu awanyimae watu nafaka,
bali baraka itamkalia kichwani kama taji
yeye aliye radhi kuiuza. 27Yeye atafutaye mema hupata ukarimu,
bali ubaya huja kwake yeye autafutaye. 28Yeyote ategemeaye utajiri wake ataanguka,
bali mwenye haki atastawi kama jani bichi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.