Mithali 11:24
Proverbs 11:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kuna mtu atoaye kwa ukarimu, hata hivyo hupata zaidi, mwingine huzuia, lakini huwa maskini.
Proverbs 11:24 in English
Proverbs 11:24 · Berean Standard Bible
One gives freely, yet gains even more; another withholds what is right, only to become poor.
Context
22Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe
ndivyo alivyo mwanamke mzuri ambaye hana busara. 23Shauku ya mwenye haki huishia tu kwenye mema,
bali tumaini la mwovu huishia tu kwenye ghadhabu. 24Kuna mtu atoaye kwa ukarimu, hata hivyo hupata zaidi,
mwingine huzuia, lakini huwa maskini. 25Mtu mkarimu atastawi;
yeye awaburudishaye wengine
ataburudishwa mwenyewe. 26Watu humlaani mtu awanyimae watu nafaka,
bali baraka itamkalia kichwani kama taji
yeye aliye radhi kuiuza.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.