Native Bible

Proverbs 10:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kumbukumbu ya mwenye haki itakuwa baraka, lakini jina la mwovu litaoza.

Proverbs 10:7 in English

Proverbs 10:7 · Berean Standard Bible

The memory of the righteous is a blessing, but the name of the wicked will rot.

Context

5Yeye akusanyaye mazao wakati wa kiangazi ni mwana mwenye hekima, lakini yeye alalaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha. 6Baraka huwa taji kichwani mwa mwenye haki, lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu. 7Kumbukumbu ya mwenye haki itakuwa baraka, lakini jina la mwovu litaoza. 8Mwenye hekima moyoni hupokea maagizo, lakini mpumbavu apayukaye huangamia. 9Mtu mwadilifu hutembea salama, lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.