Mithali 10:19
Proverbs 10:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakati maneno ni mengi, dhambi haikosekani, lakini yeye ambaye huzuia ulimi wake ni mwenye busara.
Proverbs 10:19 in English
Proverbs 10:19 · Berean Standard Bible
When words are many, sin is unavoidable, but he who restrains his lips is wise.
Context
17Anayekubali kuadibishwa yuko katika njia ya uzima,
lakini yeyote anayepuuza maonyo hupotosha wengine. 18Yeye afichaye chuki yake ana midomo ya uongo,
na yeyote anayeeneza uchonganishi ni mpumbavu. 19Wakati maneno ni mengi, dhambi haikosekani,
lakini yeye ambaye huzuia ulimi wake ni mwenye busara. 20Ulimi wa mwenye haki ni fedha iliyo bora,
bali moyo wa mwovu una thamani ndogo. 21Midomo ya mwenye haki hulisha wengi,
lakini wapumbavu hufa kwa kukosa ufahamu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.