Mithali 10:15
Proverbs 10:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome, bali ufukara ni maangamizi ya maskini.
Proverbs 10:15 in English
Proverbs 10:15 · Berean Standard Bible
The wealth of the rich man is his fortified city, but poverty is the ruin of the poor.
Context
13Hekima hupatikana katika midomo ya wenye kupambanua,
lakini fimbo ni kwa ajili ya mgongo wake asiye na ufahamu. 14Wenye hekima huhifadhi maarifa,
bali kinywa cha mpumbavu hualika maangamizi. 15Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome,
bali ufukara ni maangamizi ya maskini. 16Ujira wa wenye haki huwaletea uzima,
lakini mapato ya waovu huwaletea adhabu. 17Anayekubali kuadibishwa yuko katika njia ya uzima,
lakini yeyote anayepuuza maonyo hupotosha wengine.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.