Wafilipi 4:13
Philippians 4:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
Philippians 4:13 in English
Philippians 4:13 · Berean Standard Bible
I can do all things through Christ who gives me strength.*
Context
11Sisemi hivyo kwa vile nina mahitaji, la! Kwa maana nimejifunza kuridhika katika hali yoyote. 12Ninajua kupungukiwa, pia ninajua kuwa na vingi. Nimejifunza siri ya kuridhika katika kila hali, wakati wa kushiba na wakati wa kuona njaa, wakati wa kuwa na vingi na wakati wa kupungukiwa. 13Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. 14Lakini, mlifanya vyema kushiriki nami katika taabu zangu. 15Zaidi ya hayo, ninyi Wafilipi mnajua kwamba siku za kwanza nilipoanza kuhubiri Injili, nilipoondoka Makedonia, hakuna kanisa jingine lililoshiriki nami katika masuala ya kutoa na kupokea isipokuwa ninyi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.