Native Bible

Numbers 9:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Adhimisheni wakati ulioamriwa, yaani wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi huu, kufuatana na desturi zake zote na masharti yake.”

Numbers 9:3 in English

Numbers 9:3 · Berean Standard Bible

You are to observe it at the appointed time, at twilight on the fourteenth * day of this month, in accordance with its statutes and ordinances.”

Context

1Bwana akasema na Mose katika Jangwa la Sinai katika mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili baada ya Waisraeli kutoka Misri. Akasema, 2“Waamuru Waisraeli waadhimishe Pasaka katika wakati ulioamriwa. 3Adhimisheni wakati ulioamriwa, yaani wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi huu, kufuatana na desturi zake zote na masharti yake.” 4Hivyo Mose akawaambia Waisraeli waiadhimishe Pasaka, 5nao wakafanya hivyo kwenye Jangwa la Sinai wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza. Waisraeli wakafanya kila kitu kama vile Bwana alivyomwamuru Mose.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.