Native Bible

Numbers 8:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Utawaleta Walawi mbele za Bwana, na Waisraeli wataweka mikono yao juu ya Walawi.

Numbers 8:10 in English

Numbers 8:10 · Berean Standard Bible

You are to present the Levites before the LORD and have the Israelites lay their hands upon them.

Context

8Waambie wamchukue fahali mchanga pamoja na sadaka yake ya nafaka ya unga laini uliochanganywa na mafuta; kisha utamchukua fahali mchanga wa pili kwa ajili ya sadaka ya dhambi. 9Walete Walawi mbele ya Hema la Kukutania na ukusanye jumuiya yote ya Waisraeli. 10Utawaleta Walawi mbele za Bwana, na Waisraeli wataweka mikono yao juu ya Walawi. 11Aroni atawaweka Walawi mbele za Bwana kama sadaka ya kuinua kutoka kwa Waisraeli, ili kwamba wawe tayari kuifanya kazi ya Bwana. 12“Baada ya Walawi kuweka mikono yao juu ya vichwa vya hao mafahali wawili, tumia mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi kwa Bwana, na mwingine kuwa sadaka ya kuteketezwa, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Walawi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.