Native Bible

Numbers 8:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Walete Walawi mbele ya Hema la Kukutania na ukusanye jumuiya yote ya Waisraeli.

Numbers 8:9 in English

Numbers 8:9 · Berean Standard Bible

Bring the Levites before the Tent of Meeting and assemble the whole congregation of Israel.

Context

7Ili kuwatakasa fanya hivi: Nyunyizia maji ya utakaso juu yao; kisha uwaambie wanyoe nywele kwenye mwili mzima, wafue nguo zao na hivyo wajitakase wenyewe. 8Waambie wamchukue fahali mchanga pamoja na sadaka yake ya nafaka ya unga laini uliochanganywa na mafuta; kisha utamchukua fahali mchanga wa pili kwa ajili ya sadaka ya dhambi. 9Walete Walawi mbele ya Hema la Kukutania na ukusanye jumuiya yote ya Waisraeli. 10Utawaleta Walawi mbele za Bwana, na Waisraeli wataweka mikono yao juu ya Walawi. 11Aroni atawaweka Walawi mbele za Bwana kama sadaka ya kuinua kutoka kwa Waisraeli, ili kwamba wawe tayari kuifanya kazi ya Bwana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.