Hesabu 33:4
Numbers 33:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
waliokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza wote, ambao Bwana alikuwa amewaua katikati yao, kwa kuwa Bwana alikuwa ameleta hukumu juu ya miungu yao.
Numbers 33:4 in English
Numbers 33:4 · Berean Standard Bible
who were burying all their firstborn, whom the LORD had struck down among them; for the LORD had executed judgment against their gods.
Context
2Kwa agizo la Bwana, Mose aliweka kumbukumbu ya vituo katika safari yao. Hivi ndivyo vituo katika safari yao: 3Waisraeli walisafiri kutoka Ramesesi katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, siku iliyofuata Pasaka. Walitembea kwa ujasiri wazi mbele ya Wamisri wote, 4waliokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza wote, ambao Bwana alikuwa amewaua katikati yao, kwa kuwa Bwana alikuwa ameleta hukumu juu ya miungu yao. 5Waisraeli waliondoka Ramesesi na kupiga kambi huko Sukothi. 6Wakaondoka Sukothi na kupiga kambi huko Ethamu, pembeni mwa jangwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.