Hesabu 31:13
Numbers 31:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mose, kuhani Eleazari na viongozi wote wa jumuiya wakatoka kuwalaki nje ya kambi.
Numbers 31:13 in English
Numbers 31:13 · Berean Standard Bible
And Moses, Eleazar the priest, and all the leaders of the congregation went to meet them outside the camp.
Context
11Walichukua nyara zote na mateka, pamoja na watu na wanyama, 12nao waliwaleta wafungwa mateka na nyara kwa Mose na kwa kuhani Eleazari, nao Waisraeli walikusanyika kwenye kambi zao katika tambarare za nchi ya Moabu, kando ya Yordani ngʼambo ya Yeriko. 13Mose, kuhani Eleazari na viongozi wote wa jumuiya wakatoka kuwalaki nje ya kambi. 14Mose aliwakasirikia maafisa wa jeshi, yaani hao wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, ambao walirudi kutoka vitani. 15Mose akawauliza, “Je, mmewaacha wanawake wote hai?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.