Hesabu 3:35
Numbers 3:35 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kiongozi wa jamaa za koo za Wamerari alikuwa Surieli mwana wa Abihaili; hawa walitakiwa kuweka kambi zao upande wa kaskazini mwa Maskani.
Numbers 3:35 in English
Numbers 3:35 · Berean Standard Bible
The leader of the families of the Merarites was Zuriel son of Abihail; they were to camp on the north side of the tabernacle.
Context
33Kwa Merari kulikuwa na koo za Wamahli na Wamushi; hizi zilikuwa koo za Merari. 34Hesabu ya waume wote wenye umri wa mwaka mmoja au zaidi waliohesabiwa walikuwa 6,200. 35Kiongozi wa jamaa za koo za Wamerari alikuwa Surieli mwana wa Abihaili; hawa walitakiwa kuweka kambi zao upande wa kaskazini mwa Maskani. 36Wamerari waliwekwa kutunza miimo ya Maskani, mataruma yake, nguzo, vitako na vifaa vyake vyote na kila kitu kilichohusika na matumizi yake, 37na pia nguzo za ua unaozunguka pamoja na vitako vyake, vigingi vya hema na kamba zake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.