Native Bible

Numbers 3:37 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

na pia nguzo za ua unaozunguka pamoja na vitako vyake, vigingi vya hema na kamba zake.

Numbers 3:37 in English

Numbers 3:37 · Berean Standard Bible

as well as the posts of the surrounding courtyard with their bases, tent pegs, and ropes.

Context

35Kiongozi wa jamaa za koo za Wamerari alikuwa Surieli mwana wa Abihaili; hawa walitakiwa kuweka kambi zao upande wa kaskazini mwa Maskani. 36Wamerari waliwekwa kutunza miimo ya Maskani, mataruma yake, nguzo, vitako na vifaa vyake vyote na kila kitu kilichohusika na matumizi yake, 37na pia nguzo za ua unaozunguka pamoja na vitako vyake, vigingi vya hema na kamba zake. 38Mose, na Aroni na wanawe walitakiwa kuweka kambi zao mashariki mwa Maskani, kuelekea mawio ya jua, mbele ya Hema la Kukutania. Wao walihusika na utunzaji wa mahali patakatifu kwa niaba ya Waisraeli. Mtu mwingine yeyote aliyepasogelea mahali patakatifu angeuawa. 39Jumla ya hesabu ya Walawi waliohesabiwa na Mose na Aroni kwa amri ya Bwana, kufuatana na koo, pamoja na kila mume mwenye umri wa mwezi mmoja au zaidi, walikuwa 22,000.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.