Hesabu 24:18
Numbers 24:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Edomu itamilikiwa, Seiri, adui wake, itamilikiwa, lakini Israeli atakuwa na nguvu.
Numbers 24:18 in English
Numbers 24:18 · Berean Standard Bible
Edom will become a possession, as will Seir, his enemy; but Israel will perform with valor.
Context
16ujumbe wake yeye ambaye husikia maneno ya Mungu,
ambaye ana maarifa kutoka kwa Aliye Juu Sana,
huona maono kutoka Mwenyezi,
ambaye huanguka kifudifudi
na ambaye macho yake yamefunguka: 17“Namwona yeye, lakini si sasa;
namtazama yeye, lakini si karibu.
Nyota itatoka kwa Yakobo,
fimbo ya ufalme itainuka kutoka kwa Israeli.
Atawaponda Wamoabu vipaji vya nyuso
na mafuvu yote ya wana wa Shethi. 18Edomu itamilikiwa,
Seiri, adui wake, itamilikiwa,
lakini Israeli atakuwa na nguvu. 19Mtawala atakuja kutoka kwa Yakobo
na kuangamiza walionusurika katika mji.” 20Kisha Balaamu akawaona watu wa Amaleki, na kutoa ujumbe wake:
“Amaleki ilikuwa ya kwanza miongoni mwa mataifa,
lakini mwisho wake itaangamizwa milele.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.