Hesabu 24:16
Numbers 24:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
ujumbe wake yeye ambaye husikia maneno ya Mungu, ambaye ana maarifa kutoka kwa Aliye Juu Sana, huona maono kutoka Mwenyezi, ambaye huanguka kifudifudi na ambaye macho yake yamefunguka:
Numbers 24:16 in English
Numbers 24:16 · Berean Standard Bible
the prophecy of one who hears the words of God, who has knowledge from the Most High, who sees a vision from the Almighty, who bows down with eyes wide open:
Context
14Sasa ninarudi kwa watu wangu. Lakini njoo, nikuonye kuhusu kile watu hawa watakachowatenda watu wako siku zijazo.” 15Kisha Balaamu akatoa ujumbe wake:
“Ujumbe wa Balaamu mwana wa Beori,
ujumbe wake yeye ambaye jicho lake linaona vizuri; 16ujumbe wake yeye ambaye husikia maneno ya Mungu,
ambaye ana maarifa kutoka kwa Aliye Juu Sana,
huona maono kutoka Mwenyezi,
ambaye huanguka kifudifudi
na ambaye macho yake yamefunguka: 17“Namwona yeye, lakini si sasa;
namtazama yeye, lakini si karibu.
Nyota itatoka kwa Yakobo,
fimbo ya ufalme itainuka kutoka kwa Israeli.
Atawaponda Wamoabu vipaji vya nyuso
na mafuvu yote ya wana wa Shethi. 18Edomu itamilikiwa,
Seiri, adui wake, itamilikiwa,
lakini Israeli atakuwa na nguvu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.