Hesabu 24:14
Numbers 24:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sasa ninarudi kwa watu wangu. Lakini njoo, nikuonye kuhusu kile watu hawa watakachowatenda watu wako siku zijazo.”
Numbers 24:14 in English
Numbers 24:14 · Berean Standard Bible
Now I am going back to my people, but come, let me warn you what this people will do to your people in the days to come.”
Context
12Balaamu akamwambia Balaki, “Je, hukumbuki jinsi nilivyowaambia wajumbe uliowatuma kwangu? Niliwaambia hivi, 13‘Hata ikiwa Balaki angenipa jumba lake la kifalme likiwa limejazwa fedha na dhahabu, nisingeweza kufanya kitu chochote kwa matakwa yangu, kikiwa kizuri au kibaya, kwenda kinyume na agizo la Bwana, nami imenipasa kusema tu kile Bwana atakachosema’? 14Sasa ninarudi kwa watu wangu. Lakini njoo, nikuonye kuhusu kile watu hawa watakachowatenda watu wako siku zijazo.” 15Kisha Balaamu akatoa ujumbe wake:
“Ujumbe wa Balaamu mwana wa Beori,
ujumbe wake yeye ambaye jicho lake linaona vizuri; 16ujumbe wake yeye ambaye husikia maneno ya Mungu,
ambaye ana maarifa kutoka kwa Aliye Juu Sana,
huona maono kutoka Mwenyezi,
ambaye huanguka kifudifudi
na ambaye macho yake yamefunguka:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.