Native Bible

Numbers 23:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nimepokea agizo kubariki; amebariki, nami siwezi kubadilisha.

Numbers 23:20 in English

Numbers 23:20 · Berean Standard Bible

I have indeed received a command to bless; He has blessed, and I cannot change it.

Context

18Ndipo Balaamu akasema ujumbe wake: “Balaki, inuka na usikilize, nisikie mimi, wewe mwana wa Sipori. 19Mungu si mtu, hata aseme uongo, wala yeye si mwanadamu, hata ajute. Je, anasema, kisha asitende? Je, anaahidi, asitimize? 20Nimepokea agizo kubariki; amebariki, nami siwezi kubadilisha. 21“Haijaonekana bahati mbaya katika Yakobo, wala taabu katika Israeli. Bwana, Mungu wao yu pamoja nao, nayo sauti kuu ya Mfalme imo katikati yao. 22Mungu aliwatoa kutoka Misri; wao wana nguvu za nyati.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.