Hesabu 21:13
Numbers 21:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakasafiri kutoka hapo na kupiga kambi kando ya Mto Arnoni, ambao uko katika jangwa lililoenea hadi nchi ya Waamori. Arnoni ni mpaka wa Moabu, kati ya Moabu na Waamori.
Numbers 21:13 in English
Numbers 21:13 · Berean Standard Bible
From there they moved on and camped on the other side of the Arnon, in the wilderness that extends into the Amorite territory. Now the Arnon is the border between the Moabites and the Amorites.
Context
11Kisha wakaondoka Obothi na kupiga kambi huko Iye-Abarimu, katika jangwa linalotazamana na Moabu kuelekea mawio ya jua. 12Kutoka hapo waliendelea mbele wakapiga kambi kwenye Bonde la Zeredi. 13Wakasafiri kutoka hapo na kupiga kambi kando ya Mto Arnoni, ambao uko katika jangwa lililoenea hadi nchi ya Waamori. Arnoni ni mpaka wa Moabu, kati ya Moabu na Waamori. 14Ndiyo sababu Kitabu cha Vita vya Bwana kinasema:
“…Mji wa Wahebu nchini Seifa na mabonde
ya Arnoni, 15na miteremko ya mabonde
inayofika hadi mji wa Ari
na huelekea mpakani mwa Moabu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.