Hesabu 21:11
Numbers 21:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha wakaondoka Obothi na kupiga kambi huko Iye-Abarimu, katika jangwa linalotazamana na Moabu kuelekea mawio ya jua.
Numbers 21:11 in English
Numbers 21:11 · Berean Standard Bible
They journeyed from Oboth and camped at Iye-abarim in the wilderness opposite Moab to the east.
Context
9Kwa hiyo Mose akatengeneza nyoka wa shaba na kumweka juu ya mti. Kisha wakati mtu yeyote aliumwa na nyoka, naye akamtazama yule nyoka wa shaba, aliishi. 10Waisraeli waliendelea na safari yao na wakapiga kambi huko Obothi. 11Kisha wakaondoka Obothi na kupiga kambi huko Iye-Abarimu, katika jangwa linalotazamana na Moabu kuelekea mawio ya jua. 12Kutoka hapo waliendelea mbele wakapiga kambi kwenye Bonde la Zeredi. 13Wakasafiri kutoka hapo na kupiga kambi kando ya Mto Arnoni, ambao uko katika jangwa lililoenea hadi nchi ya Waamori. Arnoni ni mpaka wa Moabu, kati ya Moabu na Waamori.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.