Native Bible

Numbers 21:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Waisraeli waliendelea na safari yao na wakapiga kambi huko Obothi.

Numbers 21:10 in English

Numbers 21:10 · Berean Standard Bible

Then the Israelites set out and camped at Oboth.

Context

8Bwana akamwambia Mose, “Tengeneza nyoka wa shaba na umweke juu ya mti; yeyote aliyeumwa na nyoka anaweza kumtazama na akaishi tena.” 9Kwa hiyo Mose akatengeneza nyoka wa shaba na kumweka juu ya mti. Kisha wakati mtu yeyote aliumwa na nyoka, naye akamtazama yule nyoka wa shaba, aliishi. 10Waisraeli waliendelea na safari yao na wakapiga kambi huko Obothi. 11Kisha wakaondoka Obothi na kupiga kambi huko Iye-Abarimu, katika jangwa linalotazamana na Moabu kuelekea mawio ya jua. 12Kutoka hapo waliendelea mbele wakapiga kambi kwenye Bonde la Zeredi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.