Native Bible

Numbers 18:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Kila kitu katika Israeli ambacho kimetolewa kwa Bwana ni chenu.

Numbers 18:14 in English

Numbers 18:14 · Berean Standard Bible

Every devoted thing in Israel belongs to you.

Context

12“Ninawapa mafuta ya zeituni yaliyo bora kuliko yote, na divai mpya iliyo bora kuliko zote na nafaka wanazompa Bwana kama malimbuko katika mavuno yao. 13Malimbuko yote ya nchi ambayo wanamletea Bwana yatakuwa yenu. Kila mmoja nyumbani kwako ambaye ni safi kwa taratibu za Ibada anaweza kula. 14“Kila kitu katika Israeli ambacho kimetolewa kwa Bwana ni chenu. 15Kila mzaliwa wa kwanza wa mwanadamu na wa mnyama, ambaye ametolewa kwa Bwana ni wenu. Lakini ni lazima mtamkomboa kila mwana mzaliwa wa kwanza na kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa wanyama wasio safi. 16Watakapokuwa na umri wa mwezi mmoja, ni lazima mtawakomboa kwa bei ya ukombozi iliyowekwa, kwa shekeli tano* za fedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, yenye uzito wa gera ishirini.*

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.