Native Bible

Numbers 17:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ndipo Mose akaleta zile fimbo zote kwa Waisraeli wote kutoka mbele za Bwana. Wakaziangalia, na kila mtu akaichukua fimbo yake mwenyewe.

Numbers 17:9 in English

Numbers 17:9 · Berean Standard Bible

Then Moses brought out all the staffs from the LORD’s presence to all the Israelites. They saw them, and each man took his own staff.

Context

7Mose akaziweka hizo fimbo mbele za Bwana ndani ya Hema la Ushuhuda. 8Siku iliyofuata Mose aliingia kwenye Hema la Ushuhuda akaona ile fimbo ya Aroni ambayo iliwakilisha jamaa ya Lawi haikuwa tu imechipuka, bali pia ilikuwa imetoa machipukizi, kuchanua maua na kuzaa malozi. 9Ndipo Mose akaleta zile fimbo zote kwa Waisraeli wote kutoka mbele za Bwana. Wakaziangalia, na kila mtu akaichukua fimbo yake mwenyewe. 10Bwana akamwambia Mose, “Rudisha fimbo ya Aroni mbele ya Sanduku la Ushuhuda, ili ihifadhiwe kama alama kwa waasi. Hili litakomesha manungʼuniko yao dhidi yangu, ili kwamba wasife.” 11Mose akafanya kama Bwana alivyomwamuru.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.