Hesabu 17:7
Numbers 17:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mose akaziweka hizo fimbo mbele za Bwana ndani ya Hema la Ushuhuda.
Numbers 17:7 in English
Numbers 17:7 · Berean Standard Bible
Then Moses placed the staffs before the LORD in the Tent of the Testimony.
Context
5Fimbo ya mtu nitakayemchagua itachipuka, nami mwenyewe nitayakomesha haya manungʼuniko ya mara kwa mara ya Waisraeli dhidi yako.” 6Hivyo Mose akasema na Waisraeli, nao viongozi wao wakampa fimbo kumi na mbili, fimbo moja kwa ajili ya kila kabila la baba zao, nayo fimbo ya Aroni ikiwa miongoni mwa hizo. 7Mose akaziweka hizo fimbo mbele za Bwana ndani ya Hema la Ushuhuda. 8Siku iliyofuata Mose aliingia kwenye Hema la Ushuhuda akaona ile fimbo ya Aroni ambayo iliwakilisha jamaa ya Lawi haikuwa tu imechipuka, bali pia ilikuwa imetoa machipukizi, kuchanua maua na kuzaa malozi. 9Ndipo Mose akaleta zile fimbo zote kwa Waisraeli wote kutoka mbele za Bwana. Wakaziangalia, na kila mtu akaichukua fimbo yake mwenyewe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.