Native Bible

Numbers 16:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini ikiwa Bwana ataleta jambo jipya kabisa, ardhi ikifunua kinywa chake na kuwameza wao, pamoja na kila kitu kilicho mali yao, nao washuke chini kaburini* wakiwa hai, ndipo mtafahamu kuwa watu hawa wamemdharau Bwana.”

Numbers 16:30 in English

Numbers 16:30 · Berean Standard Bible

But if the LORD brings about something unprecedented, and the earth opens its mouth and swallows them and all that belongs to them so that they go down alive into Sheol, then you will know that these men have treated the LORD with contempt.”

Context

28Ndipo Mose akasema, “Hivi ndivyo mtakavyojua kuwa Bwana amenituma kufanya mambo haya, na kwamba halikuwa wazo langu. 29Ikiwa watu hawa watakufa kifo cha kawaida na kupatwa na yale ya kawaida yanayowapata wanadamu, basi Bwana hakunituma mimi. 30Lakini ikiwa Bwana ataleta jambo jipya kabisa, ardhi ikifunua kinywa chake na kuwameza wao, pamoja na kila kitu kilicho mali yao, nao washuke chini kaburini* wakiwa hai, ndipo mtafahamu kuwa watu hawa wamemdharau Bwana.” 31Mara Mose alipomaliza kusema haya yote, ardhi iliyokuwa chini yao ikapasuka, 32nchi ikafunua kinywa chake na kuwameza wao, pamoja na jamaa zao, na watu wote wa Kora na mali zao zote.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.