Native Bible

Numbers 16:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ikiwa watu hawa watakufa kifo cha kawaida na kupatwa na yale ya kawaida yanayowapata wanadamu, basi Bwana hakunituma mimi.

Numbers 16:29 in English

Numbers 16:29 · Berean Standard Bible

If these men die a natural death, or if they suffer the fate of all men, then the LORD has not sent me.

Context

27Hivyo wakaondoka karibu na mahema ya Kora, Dathani na Abiramu. Dathani na Abiramu walikuwa wametoka nje, nao walikuwa wamesimama pamoja na wake zao, watoto wao na wale wanyonyao kwenye mlango wa mahema yao. 28Ndipo Mose akasema, “Hivi ndivyo mtakavyojua kuwa Bwana amenituma kufanya mambo haya, na kwamba halikuwa wazo langu. 29Ikiwa watu hawa watakufa kifo cha kawaida na kupatwa na yale ya kawaida yanayowapata wanadamu, basi Bwana hakunituma mimi. 30Lakini ikiwa Bwana ataleta jambo jipya kabisa, ardhi ikifunua kinywa chake na kuwameza wao, pamoja na kila kitu kilicho mali yao, nao washuke chini kaburini* wakiwa hai, ndipo mtafahamu kuwa watu hawa wamemdharau Bwana.” 31Mara Mose alipomaliza kusema haya yote, ardhi iliyokuwa chini yao ikapasuka,

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.