Hesabu 16:32
Numbers 16:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
nchi ikafunua kinywa chake na kuwameza wao, pamoja na jamaa zao, na watu wote wa Kora na mali zao zote.
Numbers 16:32 in English
Numbers 16:32 · Berean Standard Bible
and the earth opened its mouth and swallowed them and their households—all Korah’s men and all their possessions.
Context
30Lakini ikiwa Bwana ataleta jambo jipya kabisa, ardhi ikifunua kinywa chake na kuwameza wao, pamoja na kila kitu kilicho mali yao, nao washuke chini kaburini* wakiwa hai, ndipo mtafahamu kuwa watu hawa wamemdharau Bwana.” 31Mara Mose alipomaliza kusema haya yote, ardhi iliyokuwa chini yao ikapasuka, 32nchi ikafunua kinywa chake na kuwameza wao, pamoja na jamaa zao, na watu wote wa Kora na mali zao zote. 33Wakashuka chini kaburini wakiwa hai, pamoja na kila kitu walichokuwa nacho; nchi ikajifunika juu yao, nao wakaangamia wakatoweka kutoka kusanyiko. 34Kutoka kilio chao, Waisraeli wote waliowazunguka walikimbia, wakipaza sauti, “Nchi inatumeza na sisi pia!”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.