Hesabu 15:5
Numbers 15:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Pamoja na kila mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa au dhabihu, andaa robo ya hini ya divai kwa sadaka ya kinywaji.
Numbers 15:5 in English
Numbers 15:5 · Berean Standard Bible
With the burnt offering or sacrifice of each lamb, you are to prepare a quarter hin of wine as a drink offering.
Context
3nanyi mkitoa sadaka za kuteketezwa kwa moto, kutoka makundi ya ngʼombe au kondoo, kama harufu nzuri inayompendeza Bwana, ikiwa ni sadaka za kuteketezwa au dhabihu, kwa ajili ya nadhiri maalum ama sadaka ya hiari au sadaka ya sikukuu zenu, 4ndipo yeye aletaye sadaka yake ataiweka mbele za Bwana sadaka ya nafaka, sehemu ya kumi ya efa* ya unga laini uliochanganywa na robo ya hini* ya mafuta. 5Pamoja na kila mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa au dhabihu, andaa robo ya hini ya divai kwa sadaka ya kinywaji. 6“ ‘Pamoja na kondoo dume andaa sadaka ya nafaka ya sehemu mbili za kumi za efa* za unga laini uliochanganywa na theluthi moja* ya hini ya mafuta, 7na theluthi moja ya hini ya divai kama sadaka ya kinywaji. Vitoe kama harufu nzuri inayompendeza Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.