Native Bible

Numbers 15:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

ndipo yeye aletaye sadaka yake ataiweka mbele za Bwana sadaka ya nafaka, sehemu ya kumi ya efa* ya unga laini uliochanganywa na robo ya hini* ya mafuta.

Numbers 15:4 in English

Numbers 15:4 · Berean Standard Bible

then the one presenting his offering to the LORD shall also present a grain offering of a tenth of an ephah of fine flour * mixed with a quarter hin of olive oil.*

Context

2“Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Baada ya ninyi kuingia katika nchi ninayowapa kama nyumbani, 3nanyi mkitoa sadaka za kuteketezwa kwa moto, kutoka makundi ya ngʼombe au kondoo, kama harufu nzuri inayompendeza Bwana, ikiwa ni sadaka za kuteketezwa au dhabihu, kwa ajili ya nadhiri maalum ama sadaka ya hiari au sadaka ya sikukuu zenu, 4ndipo yeye aletaye sadaka yake ataiweka mbele za Bwana sadaka ya nafaka, sehemu ya kumi ya efa* ya unga laini uliochanganywa na robo ya hini* ya mafuta. 5Pamoja na kila mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa au dhabihu, andaa robo ya hini ya divai kwa sadaka ya kinywaji. 6“ ‘Pamoja na kondoo dume andaa sadaka ya nafaka ya sehemu mbili za kumi za efa* za unga laini uliochanganywa na theluthi moja* ya hini ya mafuta,

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.