Hesabu 12:13
Numbers 12:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivyo Mose akamlilia Bwana akisema, “Ee Mungu, nakuomba umponye!”
Numbers 12:13 in English
Numbers 12:13 · Berean Standard Bible
So Moses cried out to the LORD, “O God, please heal her!”
Context
11Kisha Aroni akamwambia Mose, “Tafadhali, bwana wangu, usituhesabie dhambi hii ambayo tumeifanya kwa upumbavu. 12Usimwache awe kama mtoto mchanga aliyezaliwa akiwa mfu, ambaye nusu ya mwili wake imeharibika hapo atokapo katika tumbo la mama yake.” 13Hivyo Mose akamlilia Bwana akisema, “Ee Mungu, nakuomba umponye!” 14Bwana akamjibu Mose, “Je, kama baba yake angemtemea usoni, asingeona aibu kwa siku saba? Mfungie nje ya kambi kwa siku saba; baada ya hapo anaweza kurudishwa kambini.” 15Kwa hiyo Miriamu akafungiwa nje ya kambi kwa siku saba, nao watu hawakuendelea na safari mpaka aliporudishwa kambini.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.