Nahumu 3:6
Nahum 3:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitakutupia uchafu, nitakufanyia dharau na kukufanya kioja.
Nahum 3:6 in English
Nahum 3:6 · Berean Standard Bible
I will pelt you with filth and treat you with contempt; I will make a spectacle of you.
Context
4yote haya kwa sababu ya wingi wa tamaa za kahaba,
anayeshawishi, bibi wa mambo ya uchawi,
anayewatia utumwani mataifa kwa ukahaba wake
na pia jamaa za watu kwa ulozi wake. 5Bwana Mwenye Nguvu Zote anasema,
“Mimi ni kinyume na ninyi.
Nitafunika uso wako kwa gauni lako.
Nitaonyesha mataifa uchi wako
na falme aibu yako. 6Nitakutupia uchafu,
nitakufanyia dharau
na kukufanya kioja. 7Wote wanaokuona watakukimbia na kusema,
‘Ninawi ipo katika kuangamia:
ni nani atakayeomboleza kwa ajili yake?’
Nitampata wapi yeyote wa kukufariji?” 8Je, wewe ni bora kuliko No-Amoni,
uliopo katika Mto Naili,
uliozungukwa na maji?
Mto ulikuwa kinga yake,
nayo maji yalikuwa ukuta wake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.