Marko 9:4
Mark 9:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza na Yesu.
Mark 9:4 in English
Mark 9:4 · Berean Standard Bible
And Elijah and Moses appeared before them, talking with Jesus.
Context
2Baada ya siku sita, Yesu akawachukua Petro, Yakobo na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao. 3Mavazi yake yakawa na weupe wa kuzima macho, meupe kuliko ambavyo mtu yeyote duniani angaliweza kuyangʼarisha. 4Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza na Yesu. 5Petro akamwambia Yesu, “Rabi, ni vyema sisi tukae hapa. Turuhusu tujenge vibanda vitatu: kimoja chako, kingine cha Mose na kingine cha Eliya.” 6Petro hakujua aseme nini kwa maana yeye na wenzake walikuwa wameogopa sana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.