Marko 8:7
Mark 8:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Walikuwa pia na visamaki vichache, Yesu akavibariki, akawaamuru wanafunzi wake wawagawie watu.
Mark 8:7 in English
Mark 8:7 · Berean Standard Bible
They also had a few small fish, and Jesus blessed them and ordered that these be set before them as well.
Context
5Yesu akawauliza, “Mna mikate mingapi?”
Wakajibu, “Tuna mikate saba.” 6Akawaambia watu waketi chini. Akiisha kuichukua mikate saba na kushukuru, akaimega na kuwapa wanafunzi wake ili wawagawie watu. Wanafunzi wake wakafanya hivyo. 7Walikuwa pia na visamaki vichache, Yesu akavibariki, akawaamuru wanafunzi wake wawagawie watu. 8Wale watu walikula na kutosheka. Baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu saba. 9Watu waliokula walikuwa wapata 4,000. Akiisha kuwaaga,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.