Marko 8:28
Mark 8:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakamjibu, “Baadhi husema wewe ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya, na bado wengine husema wewe ni mmojawapo wa manabii.”
Mark 8:28 in English
Mark 8:28 · Berean Standard Bible
They replied, “Some say John the Baptist; others say Elijah; and still others, one of the prophets.”
Context
26Yesu akamuaga aende nyumbani kwake, akimwambia, “Hata kijijini usiingie.” 27Yesu na wanafunzi wake wakaondoka kwenda katika vijiji vya Kaisaria-Filipi. Walipokuwa njiani, Yesu akawauliza, “Watu husema mimi ni nani?” 28Wakamjibu, “Baadhi husema wewe ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya, na bado wengine husema wewe ni mmojawapo wa manabii.” 29Akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?”
Petro akajibu, “Wewe ndiwe Kristo.”* 30Yesu akawaonya wasimwambie mtu yeyote habari zake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.