Native Bible

Mark 8:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yesu akamwekea tena mikono machoni. Kisha macho yake yakafunguka, kuona kwake kukarejea naye akaona kila kitu dhahiri.

Mark 8:25 in English

Mark 8:25 · Berean Standard Bible

Once again Jesus placed His hands on the man’s eyes, and when he opened them his sight was restored, and he could see everything clearly.

Context

23Yesu akamshika mkono huyo kipofu akampeleka nje ya kijiji. Baada ya kuyatemea mate macho ya yule kipofu na kumwekea mikono, Yesu akamuuliza, “Unaona chochote?” 24Yule kipofu akaangalia, akasema, “Ninaona watu, wanaonekana kama miti inayotembea.” 25Yesu akamwekea tena mikono machoni. Kisha macho yake yakafunguka, kuona kwake kukarejea naye akaona kila kitu dhahiri. 26Yesu akamuaga aende nyumbani kwake, akimwambia, “Hata kijijini usiingie.” 27Yesu na wanafunzi wake wakaondoka kwenda katika vijiji vya Kaisaria-Filipi. Walipokuwa njiani, Yesu akawauliza, “Watu husema mimi ni nani?”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.