Native Bible

Mark 7:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Naye akawaambia, “Ninyi mnayo njia nzuri ya kukataa amri za Mungu ili mpate kuyashika mapokeo yenu!

Mark 7:9 in English

Mark 7:9 · Berean Standard Bible

He went on to say, “You neatly set aside the command of God to maintain * your own tradition.

Context

7Huniabudu bure, nayo mafundisho yao ni maagizo ya wanadamu tu.’ 8Ninyi mmeziacha amri za Mungu na kushika desturi za watu.” 9Naye akawaambia, “Ninyi mnayo njia nzuri ya kukataa amri za Mungu ili mpate kuyashika mapokeo yenu! 10Kwa mfano, Mose alisema, ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na, ‘Yeyote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.’ 11Lakini ninyi mwafundisha kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kukusaidia ni Korbani’ (yaani kimewekwa wakfu kwa Mungu),

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.