Native Bible

Mark 7:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi,

Mark 7:21 in English

Mark 7:21 · Berean Standard Bible

For from within the hearts of men come evil thoughts, sexual immorality, theft, murder, adultery,*

Context

19Mtu akila kitu hakiingii moyoni mwake bali tumboni, na baadaye hutolewa nje ya mwili wake.” (Kwa kusema hivi, Yesu alivihalalisha vyakula vyote kuwa ni “safi.”) 20Akaendelea kusema, “Kile kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. 21Kwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi, 22tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matukano, kiburi na upumbavu. 23Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, nayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.