Native Bible

Mark 5:41 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akamshika mtoto mkono, akamwambia, “Talitha koum!” * (maana yake ni, “Msichana, nakuambia: amka!”)

Mark 5:41 in English

Mark 5:41 · Berean Standard Bible

Taking her by the hand, Jesus said, “Talitha koum!” which means, “Little girl, I say to you, get up!”

Context

39Alipokwisha kuingia ndani, akawaambia, “Kwa nini mnafanya ghasia na kulia? Mtoto hajafa, bali amelala tu.” 40Wale watu wakamcheka kwa dharau. Lakini yeye akawatoa wote nje, akawachukua baba na mama wa yule mtoto, pamoja na wale wanafunzi aliokuwa nao. Wakaingia ndani mpaka pale alipokuwa yule mtoto. 41Akamshika mtoto mkono, akamwambia, “Talitha koum!” * (maana yake ni, “Msichana, nakuambia: amka!”) 42Mara yule msichana akasimama, akaanza kutembea (alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili). Walipoona haya, wakastaajabu sana. 43Yesu akawaagiza kwa ukali wasimweleze mtu yeyote jambo hilo, naye akawaambia wampe yule msichana chakula.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.