Marko 5:40
Mark 5:40 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wale watu wakamcheka kwa dharau. Lakini yeye akawatoa wote nje, akawachukua baba na mama wa yule mtoto, pamoja na wale wanafunzi aliokuwa nao. Wakaingia ndani mpaka pale alipokuwa yule mtoto.
Mark 5:40 in English
Mark 5:40 · Berean Standard Bible
And they laughed at Him. After He had put them all outside, He took the child’s father and mother and His own companions, and went in to see the child.
Context
38Walipofika nyumbani kwa yule kiongozi wa sinagogi, Yesu akaona ghasia, watu wakilia na kuomboleza kwa sauti kubwa. 39Alipokwisha kuingia ndani, akawaambia, “Kwa nini mnafanya ghasia na kulia? Mtoto hajafa, bali amelala tu.” 40Wale watu wakamcheka kwa dharau.
Lakini yeye akawatoa wote nje, akawachukua baba na mama wa yule mtoto, pamoja na wale wanafunzi aliokuwa nao. Wakaingia ndani mpaka pale alipokuwa yule mtoto. 41Akamshika mtoto mkono, akamwambia, “Talitha koum!” * (maana yake ni, “Msichana, nakuambia: amka!”) 42Mara yule msichana akasimama, akaanza kutembea (alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili). Walipoona haya, wakastaajabu sana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.