Native Bible

Mark 15:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Viongozi wa makuhani wakamshtaki kwa mambo mengi.

Mark 15:3 in English

Mark 15:3 · Berean Standard Bible

And the chief priests began to accuse Him of many things.

Context

1Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani, pamoja na wazee, walimu wa sheria na Baraza lote, wakafikia uamuzi. Wakamfunga Yesu, wakamchukua na kumkabidhi kwa Pilato. 2Pilato akamuuliza, “Je, wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe umesema.” 3Viongozi wa makuhani wakamshtaki kwa mambo mengi. 4Pilato akamuuliza tena, “Je, huna la kujibu? Tazama ni mashtaka mangapi wanayaleta juu yako.” 5Lakini Yesu hakujibu lolote, hivyo Pilato akashangaa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.