Marko 14:48
Mark 14:48 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha Yesu akawaambia, “Mmekuja na panga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyangʼanyi?
Mark 14:48 in English
Mark 14:48 · Berean Standard Bible
Jesus asked the crowd, “Have you come out with swords and clubs to arrest Me as you would an outlaw?
Context
46Wale watu wakamkamata Yesu, wakamweka chini ya ulinzi. 47Ndipo mmoja wa wale waliokuwa wamesimama karibu aliuchomoa upanga wake na kumpiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio. 48Kisha Yesu akawaambia, “Mmekuja na panga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyangʼanyi? 49Siku kwa siku nilikuwa pamoja nanyi nikifundisha Hekaluni, wala hamkunikamata. Lakini Maandiko sharti yatimie.” 50Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.