Marko 10:26
Mark 10:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wanafunzi wake wakashangaa sana. Wakaulizana wao kwa wao, “Ni nani basi awezaye kuokoka?”
Mark 10:26 in English
Mark 10:26 · Berean Standard Bible
They were even more astonished and said to one another, “Who then can be saved?”
Context
24Wanafunzi wake wakashangazwa sana na maneno hayo. Lakini Yesu akawaambia tena, “Wanangu, tazama jinsi ilivyo vigumu kwa wale wanaotumainia mali kuingia katika Ufalme wa Mungu. 25Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko mtu tajiri* kuingia katika Ufalme wa Mungu.” 26Wanafunzi wake wakashangaa sana. Wakaulizana wao kwa wao, “Ni nani basi awezaye kuokoka?” 27Yesu akawatazama, akawaambia, “Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu sivyo. Mambo yote yanawezekana kwa Mungu.” 28Ndipo Petro akamjibu, “Tazama, tumeacha kila kitu na kukufuata wewe!”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.