Marko 10:25
Mark 10:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko mtu tajiri* kuingia katika Ufalme wa Mungu.”
Mark 10:25 in English
Mark 10:25 · Berean Standard Bible
It is easier for a camel to pass through the eye of a needle than for a rich man to enter the kingdom of God.”
Context
23Yesu akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, “Itakuwa vigumu sana kwa wenye mali kuingia katika Ufalme wa Mungu!” 24Wanafunzi wake wakashangazwa sana na maneno hayo. Lakini Yesu akawaambia tena, “Wanangu, tazama jinsi ilivyo vigumu kwa wale wanaotumainia mali kuingia katika Ufalme wa Mungu. 25Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko mtu tajiri* kuingia katika Ufalme wa Mungu.” 26Wanafunzi wake wakashangaa sana. Wakaulizana wao kwa wao, “Ni nani basi awezaye kuokoka?” 27Yesu akawatazama, akawaambia, “Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu sivyo. Mambo yote yanawezekana kwa Mungu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.