Mika 7:11
Micah 7:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Siku ya kujenga kuta zako itawadia, siku ya kupanua mipaka yako.
Micah 7:11 in English
Micah 7:11 · Berean Standard Bible
The day for rebuilding your walls will come— the day for extending your boundary.
Context
9Kwa sababu nimetenda dhambi dhidi yake,
nitabeba ghadhabu ya Bwana,
mpaka atakaponitetea shauri langu
na kuithibitisha haki yangu.
Atanileta nje kwenye mwanga,
nami nitaiona haki yake. 10Kisha adui yangu ataliona
naye atafunikwa na aibu,
yule aliyeniambia,
“Yu wapi Bwana Mungu wako?”
Macho yangu yataona kuanguka kwake,
hata sasa atakanyagwa chini ya mguu
kama tope barabarani. 11Siku ya kujenga kuta zako itawadia,
siku ya kupanua mipaka yako. 12Siku hiyo watu watakuja kwako
kutoka Ashuru na miji ya Misri,
hata kutoka Misri hadi Frati
na kutoka bahari hadi bahari
na kutoka mlima hadi mlima. 13Dunia itakuwa ukiwa kwa sababu ya wakazi wake,
kwa sababu ya matunda ya matendo yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.